Sunday, 16 October 2016

SOMA HISTORIA YA MWIMBAJI NEEMA NG'ASHA

Ninaitwa Neema Ng'asha ni mzaliwa wa pili katika famili ya Ng'asha Clement,iliyopo jijini Mwanza.
Nilianza kuimba tangu nikiwa sunday school lakini  mwaka 1998 nikiwa bado binti mdogo sana  Mungu alinipika mafuta kwa njia ya ajabu sana nguvu ya Mungu ilinishukia kwa nguvu sana sitasahau siku hiyo niliimba sana.Baada ya hapo nilianza kutunga nyimbo nikaanzisha band niliyoiita Jerusalem Band nikiwa na dada yangu Martha Ng'asha Mtasha na vijana wengine pale kanisani.Baadaye mwaka 2001 nilihamia Dar-es-Salaam kwa ajili ya masomo ya elimu ya juu.Mwaka 2009 baada ya kumaliza chuo niliingia studio nikarekodi album inayoitwa "USINIPITE MWOKOZI" baada ya kurekodi album hii nilipata changamoto nyingi sana katika huduma yangu na maisha kwa ujumla lakini nilimuoana Mungu akinitia nguvu sikukata tamaa.Album hii itakuwa katika mfumo wa video hivi karibuni.


                                                     Neema Ng'asha

Mwaka 2103 nilirekodi album ya pili inayoitwa
 "TUNAE BWANA"ambayo iko tayari katika mfumo wa DVD unaweza kuangalia baadhi ya nyimbo you tube link http://youtu.be/huMa6b2jfRw na  simu.TV.
Ninamshukuru Mungu amekuwa mwema sana kwangu kila iitwapo leo ninaona anazidi kunitia nguvu na kuongeza viwango vyangu.Nashukuru Mungu kwa familia yangu imekuwa ikinitia moyo kusonga mbele.Shauku ya moyo wangu ni kuona ninafikia nyanja ya kimataifa nizidi kuutangaza wema wa Mungu  na  matendo yake makuu.
Nina maono ya kuwasaidia vijana walio na huduma ya uimbaji maana najua na mimi Mungu alinipa hii huduma bado nikiwa mdogo sana nimekutana na changamoto nyingi za kukatishwa tamaa makanisani na changamoto za maisha  lakini nilimlilia Mungu hata hapa nilipofikia leo Mungu amekuwa EBENEZA kwangu.
Neema Ng'asha Mwamba.

No comments:

Post a Comment