Sunday, 16 October 2016

JOSHUA MAKONDEKO AWAJIA JUU CHAMA CHA MUZIKI WA INJILI,NI BAADA YA KUTOONEKANA KWENYE MSIBA WA MKE WA JACKSON BENTY

Mwimbaji wa muziki wa Inili Tanzania, Joshua Makondeko ameonyesha kuchukizwa na kitendo cha chama cha muziki wa Injili Tanzania (CHAMUITA) makao makuu kutoonyesha ushirikiano kwa mwimbaji Jackson Benty ambaye siku chache zilizopita amefiwa na mke wake, Winnie Jackson Benty.
Kupitia ukarasa wake wa facebook, Makondeko ameeleza jinsi yeye na waimbaji wachache kama Dunstan Mtoi naEmanuel Mabisa walivyojitoa na kwenda kwenye mazishi ya mke wa mwimbaji huyo huku uongozi wa chama hicho kwa upande wa makao makuu wakitoa ushirikiano hafifu.
Kwa upande mwingine Joshua Makondeko amepongeza wanachama wa chama hicho kanda ya kaskazini kwa kuwa mstari wa mbele kwenye msiba huo na kuongeza kuwa hata mwimbaji Stella Joel (katibu mwenezi wa CHAMUITAmakao  makuu) alipofiwa na mume wake watu wa kanda ya kaskazini walishiriki kikamilifu tofauti na makao makuu walivyoshiriki kwa Benty ambaye yupo kanda ya kaskazini.
Hivi ndivyo Makondeko alivyoandika kwenye ukarasa wake wa facebook..
Kwa Pamoja tulifanikiwa kumzika Mke wa Mwimbaji Mwenzetu Jackson Benty. 
Kwa kujali dhana ya Upendo na Umoja toka Moyoni,Mimi Emanuel Mabisa na Dastan Mtoi tuliamua Kuwawakilisha Waimbaji wote Tz Nzima kwa garama zetu,Japo kwa Uchovu Mwingi bila Mapumziko ila Niliamua kuunganisha Arusha Usiku kwa Usiku. 
Najiuliza swaLi: ~hivi ninini Kazi ya”” CHAMUITA” Makao Makuu??…Jukumu Lao ninini??..Ni Majungu,Wivu tu na Ugomvi??
Ikiwa msiba kama huu unatokea halafu responde na Responsible inakuwa hafifu hivyo??…Japo Sitaki kuamini kama Waimbaji wana Tatizo la kutokufanya wanachoambiwa,ila Wanatarajia Maelekezo toka kwa wahusika na Uwajibikaji..Nakumbuka Mume wa Stella JoeL alivyokufa Waimbaji Kanda ya Kaskazini walitoa Mchango na wakatuma wawakilishi kuja knye Mazishi..Je ina Maana sisi ndio bora Zaidi Yao???Jukumu La Makao Makuu Liko Wapi???
Hongera nyingi na Shukrani kwa WanachaMuita Kanda ya Kaskazini, Uongozi wenu,Umoja wenu na Kujitoa kwenu, Tunauona, Tunaupenda na Inaleta ladha ya kuitwa wana Wa Lawi..Mtu asiwagombanishe wala Msiache Umoja huo. Mnastahili kuwa Makao Makuu Dar. Na wale wa Makao Makuu wapelekwe WiLayA ya Katavi..
Shukrani nyingi Waziri wa Mambo ya Ndani Rafiki yangu Mhe. MwiguLu Nchemba na Grace Product Nilipowaambia tu hamkusita kutuma rambirambi zanu.
#TutapitaKatikatiYaoNoLiMiT”

No comments:

Post a Comment