Wednesday, 7 December 2016


BEN BONGE CONCERT


Mwambaji wa nyimbo za injili Tanzania benjamin jacon almaarufu kama bishop ben bonge anataraja kufanya uzinduzi tarehe18/12/2016  T.A.G MANZESE B MABIBO MAKUTANO HI SIO YA KUKOSA.

Saturday, 12 November 2016

UZINDUZI UZINDUZI UZINDUZI.

Lightness Vicent ni Muimbaji wa Nyimbo za injili hapa nchini Tanzania ni Muimbaji mwenye kipaji na huduma kubwa ya uimbaji TAFADHALI usikose kufika kwenye uzinduzi wa album yake Mpya inayojulikana kwa jina la SITASUMBUKA uzinduzi utafanyika tar 13 Nov jumapili hii katia kanisa la John Saidi lililopo Ubungo External.Kazi hii imefanyika chini ya kampuni kubwa Tanzania Smart visual Productions chini ya Director David James

Friday, 4 November 2016

MWANAMKE KUBALI YESU AKUHUDUMIE.
Winging ladie mwanza wakishirikiana na kamati ya maandalizi na mbeba maono Rose Shaboka wanakuletea semina ya kina mama na mabinti itakayo fanyika tarehe 22 na 23 mahali ni victoria palace hotel hakuna kiingilio isipokuwa 10000 tu kwa jili ya chakula chako njoo ujifunze jinsi ya kuwa binti na mwanamke wa tofauti wanenaji ni mbeba maono Rose shaboka kutoka Dar na Mwalimu Irene Mbowe toka Arusha

(Gospel News) Atosha Kissava aja na 4g ya featuring.


Star wa muziki wa injili Atosha Kissava anayetamba na wimbo wake wa U mwema ameelezea baadhi ya mipango yake ambayo ameiandaa kwa mwaka 2017, Atosha amesema kuwa kati ya mipango aliyonayo ni kufanya kolabo za kutosha kwa waimbaji wa Tanzania na walio nje ya mipaka ya Tanzania hivyo wadau wake wakae tayari kwa ujio wa makolabo ya nguvu kutoka kwa Atosha Kissava

SARAH MVUNGI TOKA 2012.

Katika tasnia ya muziki wa injili ndani ya miaka hii miwili kumeonekana kuwa na mabadiliko makubwa ambapo waimbaji wengi wamekuwa wakijituma kwa kufanya video yenye kuendana na wakati tulionao na nikitu kilichowafanya waimbaji wengi kuwa bize sana na location lakini suala hilo limekuwa tofauti kwa upande wa mwimbaji Sarah Mvungi ambaye yeye ametuambia kuwa mara ya mwisho kwenda location na kusimama mbele ya camera kwa ajili ya kushoot ilikuwa mwaka 2012 wakati alipokuwa akifanya album yake ya Niacheni Nimfuate Yesu hadi sasa mwaka 2016 mwishoni haijui camera yeyote

FROLA MBASHA ABADILISHA JINA RASMI SOMA HAPA JINA LAKE JIPYA



Mwimbaji mkongwe wa muziki wa injili aliyekuwa akifahamika kwa jina la Flora Mbasha week hii amebadilisha rasmi jina lake na kulitambulisha jina lake jipya la Madam Flora ambalo atakuwa akilitumia katika shughuli zake mbali mbali pamoja na brand yake ya kimuziki Pia Madam Flora amesema amekaa kimya kwa muda mrefu bila kuachia kazi yeyote sasa ameamua kurudi rasmi na kwa sasa ameachia wimbo wake mpya unaoitwa Wakati Wake ambao unafanya vizuri katika media mbali mbali za ndani na nje ya mipaka ya Tanzania